Vitabu milioni 1.4 vimeuzwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu Tehran
(last modified Tue, 20 May 2025 06:24:52 GMT )
May 20, 2025 06:24 UTC
  • Vitabu milioni 1.4 vimeuzwa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu Tehran

Maonyesho ya 36 ya Kimataifa ya Vitabu Tehran ambayo yalimalizika Jumamosi jioni, yalivutia zaidi ya wageni milioni sita katika kipindi cha siku 11 za maonyesho.

Takwimu za mwisho zilizotolewa katika hafla ya kufunga zilionyesha kuwa mauzo yalifikia zaidi ya dola milioni 8, kupitia majukwaa ya ana kwa ana na mtandaoni.

Aidha zaidi ya vitabu milioni 1.4 viliuzwa katika maonyesho hayo, ambayo yalifunguliwa Mei 7 chini ya kaulimbiu “Tusome kwa Ajili ya Iran”.

Maonyesho ya mwaka huu yalishuhudia mwelekeo mkubwa kuelekea mauzo ya mtandaoni, ambayo yaliongezeka kwa asilimia 38 kutoka mwaka uliopita na kwa mara ya kwanza yakazidi mauzo ya ana kwa ana.

Msemaji wa maonyesho hayo, Ebrahim Heidari, alielezea tukio  hili kama “mabadiliko makubwa” katika tabia ya wasomaji.

Wachapishaji wa vitabu vya afya, lishe, saikolojia, na sayansi ya michezo walionyesha uwepo mkubwa. Kwa mujibu wa waandaaji, sekta hizi zilikuwa “zimeonekana zaidi kuliko wakati wowote”.

Kuongezeka kwa machapisho yanayohusu maisha yenye afya na ustawi kunaashiria ongezeko la hamu miongoni mwa Wairani katika kuendesha  maisha kwa kutegemea maarifa.

Moja ya vibanda vilivyotembelewa zaidi kilikuwa cha Hatami Publishing, ambacho kilikuwa na vitabu kuhusu afya ya akili, lishe, na sayansi ya michezo.

Ongezeko la idadi ya watu katika vibanda vinavyohusiana na afya linaonyesha kile ambacho mchapishaji mmoja alikiita “hatua dhahiri” kuelekea umma katika mada zinazohusiana na ustawi wa kimwili na kiakili.