Araqchi: IAEA ‘imeridhishwa kikamilifu’ na makubaliano ya ushirikiano
Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) umeridhishwa kikamilifu na vipengee vya makubaliano yaliyofikiwa karibuni kati ya wakala huo na Jamhuri ya Kiislamu.
"Kuanzia sasa, Ushirikiano wa Iran na IAEA utafuata fremu hii, na wakala huo umeridhishwa kikamilifu na makubaliano hayo. Sayyid Abbas Araqchi ameeleza haya jana katika mazungumzo na waandishi wa habari akiwa pamona na waziri mwenzake wa Tunisnia, Mohamed Ali Nafti.
Araqchi alielekea Tunis baada ya kutia saini makubaliano haya tajwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi mjini Cairo,Misri siku moja mapema ili kuandaa njia ya kuanza tena ushirikiano kati ya pande mbili.
Tehran ilisitisha ushirikiano na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) katika kupinga azimio la hivi karibuni la wakala huo wa nyuklia dhidi ya Iran ambalo mwezi Juni mwak ahuu lilitumiwa na utawala wa Israel na Marekani kujaribu kuhalalisha vita vyao haramu dhidi ya Iran.
Akizungumza pamoja na Grossi wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kuhitimishwa kwa makubaliano hayo, Araqchi alibainisha namna ushirikiano wa Iran katika kufikia makubaliano hayo ulivyodhihirisha nia njema ya nchi nchi, licha ya kukabiliwa na uchokozi.