Moscow: Kurejeshwa vikwazo dhidi ya Iran sio halali kisheria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i131028-moscow_kurejeshwa_vikwazo_dhidi_ya_iran_sio_halali_kisheria
Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa alisema Ijumaa jioni kwamba, kurejeshwa kwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hakuna uhalali wowote wa kisheria na kwamba waliotia saini makubaliano ya nyuklia hawapaswi kuchukua hatua kama hiyo.
(last modified 2025-09-20T11:25:35+00:00 )
Sep 20, 2025 11:25 UTC
  • Moscow: Kurejeshwa vikwazo dhidi ya Iran sio halali kisheria

Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa alisema Ijumaa jioni kwamba, kurejeshwa kwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hakuna uhalali wowote wa kisheria na kwamba waliotia saini makubaliano ya nyuklia hawapaswi kuchukua hatua kama hiyo.

Vasily Nebenzia, ​​mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu utaratibu wa Snapback, alisema: "Nchi zilizotia saini makubaliano ya nyuklia ya Iran hazina haki ya kurudisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hii." Akizungumzia hatua ya nchi tatu za Ulaya yaani Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, kuhusu kuamilisha utaratibu wa snapback, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Russia amesema: "Hatua ya Troika ya Ulaya ya kuweka tena vikwazo dhidi ya Iran haina msingi wowte wa kisheria." Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi za Magharibi zinapinga diplomasia kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, na kwamba kurudishwa vikwazo dhidi ya Iran ni aina ya ulaghai dhidi ya nchi huru inayojitawala.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Russia amesisitiza kwa kusema: 'Rasimu ya azimio lililojadiliwa Ijumaa ni ukiukaji wa wazi wa azimio nambari 2231 na makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA, na Moscow haitambui kurejeshwa kwa vikwazo hivyo."