Iran, Misri zaafiki kuendeleza mazungumzo ya kupanua uhusiano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i134012-iran_misri_zaafiki_kuendeleza_mazungumzo_ya_kupanua_uhusiano
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Misri wameafiki juu ya kuweko mazungumzo ya kupanua uhusiano wa mataifa yao.
(last modified 2025-12-07T05:42:24+00:00 )
Dec 07, 2025 03:41 UTC
  • Iran, Misri zaafiki kuendeleza mazungumzo ya kupanua uhusiano
    Iran, Misri zaafiki kuendeleza mazungumzo ya kupanua uhusiano

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Misri wameafiki juu ya kuweko mazungumzo ya kupanua uhusiano wa mataifa yao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kujadili uhusiano wa pande mbili na matukio ya hivi karibuni ya kikanda na kukubaliana kuendelea na mazungumzo yenye lengo la kuimarisha uhusiano.

Mazungumzo hayo yanafanyika wakati Tehran na Cairo zikiendeleza kwa tahadhari juhudi za kuleta utulivu na kupanua ushirikiano wao wa kidiplomasia huku kukiwa na mvutano unaoongezeka huko Gaza na Lebanon kutokana na kuendelea ukwamishaji mambo wa Israel na ukiukaji wake wa mara kwa mara wa kusitisha mapigano.

Iran na Misri, wahusika wakuu wawili wa kikanda, wamezidi kuratibu juu ya majibu ya kibinadamu na kisiasa kwa mashambulio yanayoendelea ya Israel. Mazungumzo yao yana athari kubwa kwa diplomasia ya kikanda.

Pande hizo "zimesisitiza ulazima wa kuchukuliwa hatua za haraka na jamii ya kimataifa kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni," zikibainisha ukiukaji wa mara kwa mara wa kusitisha mapigano na mashambulizi yanayoendelea.

Msisitizo juu ya Lebanon na Gaza unaonyesha wasiwasi unaoongezeka katika eneo lote wakati Israel inazidisha operesheni na inakabiliwa na shutuma za kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano. Iran na Misri zimekuwa miongoni mwa mataifa yanayoshinikiza uingiliaji kati wa haraka wa kimataifa ili kukomesha mauaji ya raia.