Velayati: Iran mbeba bendera ya Uislamu duniani
(last modified Tue, 16 Feb 2016 08:18:55 GMT )
Feb 16, 2016 08:18 UTC
  • Velayati: Iran mbeba bendera ya Uislamu duniani

Dakta Ali Akbar Velayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiye mbeba bendera wa Uislamu na Waislamu duniani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran IRNA, Velayati aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho "Historia ya Jadi na ya Sasa ya Ardhi ya Iran" na sehemu ya kwanza ya ensaiklopidia kuhusu "Utamaduni na Ustaarabu wa Iran". Velayati amesema hakuna nchi yoyote iliyotoa mchango mkubwa katika kuupa nguvu, kuutangaza na kuuheshimu utamduni wa Kiislamu kama Iran ya Kiislamu. Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema katika kipindi cha kati ya miaka 200 na 300 iliyopita, Wairani wamekuwa wamebeba bendera ya wadumishaji wa mwamko wa Kiislamu duniani. Wakati huo huo, Dakta Velayati amewapongeza wananchi wa Iran kwa kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya 22 Bahman (11 Februari) kwa mnasaba wa kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Tags