Iran yavunja rekodi ya uzalishaji wa zao la ngano
Naibu Waziri wa Jihadi ya Kilimo anayesimamia masuala ya uzalishaji wa mazao nchini Iran ametangaza kuvunjwa rekodi ya uzalishaji wa ngano akisema: “Mwaka huu, kwa mara ya kwanza katika historia, taifa hili limefanikiwa kuzalisha tani milioni 14.1 za ngano nchini, kiwango ambacho kinachukuliwa kuwa kikubwa na cha kuzingatiwa.
Majid Anajafi amesema hayo katika mkutano wa 32 wa kila mwaka wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Kutegemea Mvua nchini Iran na kueleza kwamba, utendaji wa sekta ya kilimo katika uzalishaji wa mazao ya msingi umekuwa wa mafanikio makubwa na wenye umuhimu mkubwa.
Aliongeza kuwa mwenendo uliopo unaonyesha kwamb,a tija na ongezeko la uzalishaji katika sekta ya kilimo vinaendelea kuimarika, huku uzalishaji wa ngano uliofikia tani milioni 14.1 ukiwa ni ushahidi wa hali hiyo.
Aidha, alisema kuwa kwa sasa asilimia 85 ya mahitaji ya chakula ya Iran huzalishwa ndani ya nchi, huku asilimia 15 pekee ya bidhaa za chakula ikipatikana kupitia uagizaji kutoka nje. Alisema jambo hilo linaonyesha uwezo mkubwa wa sekta ya kilimo katika kuhakikisha usalama wa chakula nchini.
Naibu Waziri wa Jihadi ya Kilimo anayesimamia masuala ya uzalishaji wa mazao nchini Iran ameeleza hali ngumu iliyoikabili sekta ya kilimo mwaka uliopita kutokana na ukame, akisema kuwa, licha ya ukame huo, mgawanyo usio mzuri wa mvua, matatizo ya kiuchumi, vikwazo na hali iliyosababishwa na vita vya kulazimishwa, juhudi na ushirikiano kati ya wakulima, watafiti, wataalamu na viongozi uliwezesha uzalishaji wa mazao ya kilimo na bustani nchini kuongezeka kwa jumla ya tani milioni saba.
Iran ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa ngano katika Mashariki ya Kati, ingawa kiwango cha uzalishaji hubadilika sana kulingana na mvua na upatikanaji wa maji.
Iran ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa ngano katika Mashariki ya Kati, ikiwa na takriban tani milioni 16 kwa mwaka.