Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lapata mafanikio mengine
(last modified Mon, 29 Aug 2016 14:30:06 GMT )
Aug 29, 2016 14:30 UTC
  • Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lapata mafanikio mengine

Kamanda wa kituo cha ulinzi wa anga cha Khatamul-Anbiya cha jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kufanyiwa majaribio rada ya kisasa kwa jina la Nazir.

Brigedia Jenerali Farzad Ismaili amesema leo rada hiyo ya aina yake ya Nazir imefanyiwa majaribio na kwa msingi huo hakuna ndege yoyote inayoweza kupenya katika anga ya Iran ya Kiislamu bila ya ruhusa.

Brigedia Jenerali Ismaili amesema kuwa rada ya Nazir iliyoundwa hapa nchini ni maalumu kwa kutambua vyombo vidogo vinavyoruka angani kama vile ndege za ujasusi na zisizo na rubani za mq1, rq4 na u2 na inaweza pia kwa urahisi kuyaona makombora ya balistiki na kruzi; na muhimu kuliko yote rada hii inaweza kutambua ndege zisizoweza kuonekana kwenye rada.

Mfano wa Rada ya Nazir iliyofanyiwa majaribio na Iran

Brigedia Generali Ismaili ameongeza kuwa mfumo wa rada hiyo yenye nguvu ya Nazir imefanyiwa majaribio katika umbali wa zaidi ya mita 3000 katika eneo la jangwani hapa nchini. Mfumo huu wa rada ya Nazir unaweza kupenya umbali wa kilomita kadhaa nje ya mipaka ya anga ya Iran na kutambua vitisho vyovyote vinavyotaka kuinyemelea nchi hii na kisha kutoa taarifa kwa kanali husika ya mfumo wa ulinzi.