Mnyanyua vyuma Muirani avunja rekodi mara tatu, apata dhahabu Paralympiki Rio
Muirani mnyanyua vyuma katika uzani wa juu zaidi amevunja rekodi tatu za dunia na kupata medali ya dhahabu katika Michezo ya Olyimpiki ya walemavu- Paralympiki-huko Rio de Janeiro, Brazil.
Katika jaribio lake la kwanza la kategoria ya kilo 107+, Siamand Rahman alinyanyua kila 270 na kuvunja rekodi ya Paralimipiki siku ya Jumatano katika ukumbi wa Riocentro.
Muirani huyo aliye na umri wa miaka 28 kisha alinyanyua kilo 300 na baadaye kilo 305 na hivyo kuvunja rekodi yake ya dunia ya kilo 296 na kwa utaratibu huo, akaipa Iran medali yake ya sita ya dhahabu katika Michezo ya Paralympiki.

Siamand Rahman ambaye anaiwakilisha Iran kwa mara ya pili katika Michezo ya Paralympiki, kisha aliomba kunyanya vyuma vyenye uzani wa kilo 310, baada ya kukamilisha unyanyuaji mara tatu uliohitajika katika mashindano, na hapo tena akapata mafanikio makubwa.