Rais Rouhani: Iran inapambana na magaidi kwa nguvu kubwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i16255-rais_rouhani_iran_inapambana_na_magaidi_kwa_nguvu_kubwa
Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapambana na ugaidi kwa nguvu kubwa katika eneo na dunia nzima kwa jumla.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 28, 2016 10:21 UTC
  • Rais Rouhani: Iran inapambana na magaidi kwa nguvu kubwa

Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapambana na ugaidi kwa nguvu kubwa katika eneo na dunia nzima kwa jumla.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo Jumatano alipohutubia halaiki kubwa ya watu katika mji wa Qazvin kaskazini magharibi mwa Iran.

Ameongeza kuwa, 'zimepita zile siku ambazo Iran ilikuwa ikituhumiwa kuwa eti inaunga mkono ugaidi na Wairani kutuhumiwa kuwa wanategeneza mabomu ya nyuklia lakini sasa utambulisho sahihi wa Iran umeibainikia dunia.'

Wananchi wakisikiliza hotuba ya Rais Rouhani mjini Qazvin, 28/9/2016

Rais Rouhani amesema tokea mwezi Machi mwaka huu, amekutana na viongozi 22 wa nchi mbali mbali duniani ambao wote wameipongeza nchi hii kwa kudumisha mshikamano wa kitaifa mbele ya madola ya kibeberu. Amesema viongozi wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote wamesema mafanikio ya Iran katika kufikia mapatano ya nyuklia ni mafanikio ni ya nchi zinazostawi pia.

Rais Rouhani amesema katika mapatano ya nyuklia ya Julai mwaka 2015, si tu kuwa serikali ilitetea haki za watu wa Iran bali pia haki za mataifa yote duniani yanayopigania uhuru na kujitegemea.