Rais Rouhani awasili ziarani Vietnam
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i16810-rais_rouhani_awasili_ziarani_vietnam
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili Hanoi mji mkuu wa Vietnam kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 05, 2016 11:35 UTC
  • Rais Rouhani awasili ziarani Vietnam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili Hanoi mji mkuu wa Vietnam kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo.

Rais Hassan Rouhani leo alasiri amewasili Hanoi mji mkuu wa Vietnam na kulakiwa na viongozi wa nchi hiyo na maafisa wa ubalozi wa Iran huko Vietnam ambayo ni nchi ya kwanza aliyoanza kuitembelea katika ziara yake katika nchi kadhaa za kusini mashariki mwa Asia. Rais wa Iran ameongozana na ujumbe wa kisiasa na kiuchumi wa nchi hii huko Vietnam.

Rais Hassan Rouhani akiagwa na viongozi wa ngazi ya juu kabla ya kuanza safari

Katika  ziara hiyo, Rais Rouhani ameongozana na Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje, Mahmoud Hujjati Waziri wa Jihadi ya Kilimo na Muhammad Reza Neematzadeh  Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara pamoja na Waliullah Seif Gavana wa Benki Kuu ya Iran. Ujumbe wa Iran leo hautakuwa na ratiba yoyote ya mazungumzo, hata hivyo ujumbe wa kiuchumi na sekta binafsi ya Iran ambao uliwasili mapema huko Vietnam, utaendelea na mazungumzo  yake na jumbe za Vietnam. Hapo kesho Rais Tran Dai Kuang wa Vietnam atamlaki rasmi Rais wa Iran katika ikulu yake na kisha marais hao wataanza mazungumzo.