Jacob Zuma kutembelea Iran karibuni hivi
Mtandao mmoja wa habari wa Afrika Kusini umesema kuwa, Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo anatarajiwa kutembelea Iran mwishoni mwa mwezi huu wa Februari.
Mtandao wa habari wa Moneyweb umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, lengo la safari ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini nchini Iran ni kustawisha uhusiano wa kiuchumi wa nchi hizi mbili.
Mtandao huo wa habari umeongeza kuwa, kuanza kutekelezwa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 na kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran kumetoa fursa kwa Afrika Kusini kuimarisha zaidi uhusiano wake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Vile vile umetoa ripoti kuhusu maendeleo na vivutio vya kiuchumi vya Iran na kuongeza kuwa, Iran ni fursa kubwa zaidi ya kibiashara kwa mwaka 2016 na kwamba Afrika Kusini imeamua kutumia vizuri fursa hiyo.