Ayatullah Amoli Larijani: Syria si mahala salama tena kwa magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i21760-ayatullah_amoli_larijani_syria_si_mahala_salama_tena_kwa_magaidi
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, Syria si mahala salama tena kwa magaidi na waungaji mkono wao wa Mashariki ya Kati na wa nje ya eneo hili.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Dec 19, 2016 23:36 UTC
  • Ayatullah Amoli Larijani: Syria si mahala salama tena kwa magaidi

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, Syria si mahala salama tena kwa magaidi na waungaji mkono wao wa Mashariki ya Kati na wa nje ya eneo hili.

Ayatullah Sadeq Amoli Larijani alisema hayo jana Jumatatu katika kikao na maafisa wa ngazi za juu wa idara ya mahakama hapa nchini ambapo aliashiria  hatua ya madola ya Magharibi ya kupotosha mambo katika Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa, Wamagharibi wakiwa umbali wa maelfu ya kilomita wamekuwa wakiwatuma magaidi katika eneo hili na kisha kuwapa himaya na uungaji mkono wa hali na mali.

Magaidi wa Daesh wakiwa tayari kufanya mauaji ya kikatili

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amebainisha kwamba, baadhi ya nchi zenye fikra butu katika Mashariki ya Kati nazo kwa muda mrefu sasa zimekuwa zikizusha mifarakano baina ya mataifa na kuwafanya magaidi wawaue raia wasio na hatia wa Iraq na Syria.

Ayatullah Amoli Larijani aidha amesema kuwa, miamala ya kindumakuwili na unafiki wa madola ya Magharibi katika kuamiliana na magaidi ilishadidi zaidi wakati madola hayo yalipowagawa magaidi katika makundi mawili ya magaidi wazuri na wabaya.

Aidha mkuu huyo wa Idara ya Mahakama nchini Iran amesisitiza kwamba, himaya ya madola ya Magharibi kwa magaidi ni ujumbe mbaya kabisa wa haki za binadamu ulimwenguni; na suala la haki za binadamu hii leo ulimwenguni limegeuzwa na kuwa wenzo wa kuyashinikiza baadhi ya matiafa ya Mashariki ya Kati na ulimwenguni kwa ujumla.