Iran; Mwenyekiti wa kundi la 77 la UN
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25598-iran_mwenyekiti_wa_kundi_la_77_la_un
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechukua uwenyekiti wa nchi za kundi la 77 la Umoja wa Mataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2017 23:10 UTC
  • Iran; Mwenyekiti wa kundi la 77 la UN

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imechukua uwenyekiti wa nchi za kundi la 77 la Umoja wa Mataifa.

Shirika la Habari la Sauti na Televisheni ya Iran limeripoti kuwa Reza Najafi Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yake Vienna Austria, amekuwa Mwenyekiti wa nchi za kundi la 77 la Umoja wa Mataifa huko Vienna kwa muda wa mwaka mmoja.

Balozi Reza Najafi, Mwenyekiti wa kundi la 77

Kundi la 77, ni taasisi kubwa ya kiserikali inayoundwa na nchi zinazostawi ndani ya Umoja wa Matifa. Kundi la 77 liliasisiwa rasmi mwezi Juni mwaka 1964 kwa kusainiwa hati iliyopewa jina la 'Taarifa ya pamoja ya nchi 77' na nchi 77 zinazoendelea mwishoni mwa kikao cha kwanza cha mkutano wa Biashara na Ustawi wa Umoja wa Mataifa UNCTAD huko mjini Geneva Uswisi.