Usafirishaji nje bidhaa za Iran wapiku kiwango cha uingizaji bidhaa kutoka nje
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i27380-usafirishaji_nje_bidhaa_za_iran_wapiku_kiwango_cha_uingizaji_bidhaa_kutoka_nje
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwaka jana, kiwango cha usafirishaji nje bidhaa za Iran kimekipiku kiwango cha kuingiza bidhaa kutoka nje ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 63 ya uchumi wa Iran. Amesema, hayo ni katika matunda mazuri ya uchumi wa muqawama.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Apr 06, 2017 10:18 UTC
  • Usafirishaji nje bidhaa za Iran wapiku kiwango cha uingizaji bidhaa kutoka nje

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa mwaka jana, kiwango cha usafirishaji nje bidhaa za Iran kimekipiku kiwango cha kuingiza bidhaa kutoka nje ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 63 ya uchumi wa Iran. Amesema, hayo ni katika matunda mazuri ya uchumi wa muqawama.

Rais Rouhani amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa miradi 18 ya maendeleo katika mkoa wa Semnan wa kaskazini mwa Iran na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa takwimu hizo, bidhaa zisizo za mafuta za Iran zilizosafirishwa nje ya nchi katika mwezi wa Machi zina thamani ya dola bilioni 43 na milioni 900 wakati ambapo bidhaa zilizoingizwa nchini katika mwezi huo zina thamani ya dola bilioni 43 na milioni 600 zikiwa na tofauti ya dola milioni 300 ikilinganishwa na zile zilizosafirishwa nje ya nchi.

Amesema, kaulimbiu ya mwaka huu (wa Kiirani wa Hijria Shamsia) ni "Uchumi wa Muqawama, Uzalishaji na Ajira" hivyo inabidi kaulimbiui hiyo itekelezwe kivitendo kwa kuzalisha nafasi laki saba za ajira kwa ajili ya wananchi.

Uchumi wa muqawama ni uchumi wa kutegemea nguvu za ndani

Rais Rouhani ameongeza kuwa, mwaka uliopita kiwango cha uzalishaji ajira kilikuwa kizuri kiasi fulani nchini Iran kiasi kwamba serikali ilifanikiwa kuzalisha ajira laki saba na 14 elfu mwaka huo.

Vile vile amesema, juhudi kubwa zimefanyika za kuleta ustawi katika mikoa yote ya Iran na kwamba wananchi, Bunge, Mahakama na vikosi vya ulinzi vinapaswa kutumia uwezo wao mkubwa kuisaidia Serikali katika jukumu hilo.