Ongezeko la bidhaa za Iran zinazouzwa Somalia
Kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la bidhaa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinazouzwa nchini Somalia.
Kwa mujibu wa Shirika la Ustawishaji Mauzo ya Nje nchini Iran, katika mwaka wa 2016, Iran iliuza bidhaa zenye tahamani ya dola milioni 30 nchini Somalia ikiwa ni ongezeko la asilimia 38 katika mwaka 2015.
Kwa mujibu wa Mehrdad Falah, Mkuu wa Idara ya Afrika katika Shirika la Ustawishaji Mauzo ya Nje nchini Iran, katika mwaka 2015, bidhaa za Iran zilizouzwa Somalia zilikuwa na thamani ya dola milioni 22. Ameongeza kuwa aghalabu ya bidhaa za Iran zinazouzwa Somalia ni pamoja na aina ya plasitiki ijulikanyokama Polyvinyl chloride, simiti au seruji nyeupe, biskwiti, seramiki, lami,dawa na vyombo vya chakula.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa ongezeko la bidhaa za Iran zinazouzwa Afrika.
Mwezi uliopita, Kenya ilitangazwa kuwa nchi ya Afrika inayoongoza katika ununuzi wa bidhaa kutoka Iran barani na ya 15 kwa ujumla katika ununuzi wa bidhaa za Iran duniani.
Mwambata wa kibiashara wa Iran mjini Nairobi Murtadha Daylan alisema, "Kenya ni nchi ya 15 yenye kununua bidhaa kwa wingi kutoka Iran kwa mujibu wa takwimu za mwezi Machi mwaka 2017."