Wairani kufanya maandamano kulaani jinai dhidi ya Wapalestina, Warohingya
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i32286-wairani_kufanya_maandamano_kulaani_jinai_dhidi_ya_wapalestina_warohingya
Wairani wa matabaka yote Ijumaa ijayo wanatazamiwa kufanya maandamano ya nchi nzima kulaani ukatili unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika mji mtakatifu wa Quds na Msikiti wa al Aqsa sambamba na jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wa Rohingya.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jul 26, 2017 03:34 UTC
  • Wairani kufanya maandamano kulaani jinai dhidi ya Wapalestina, Warohingya

Wairani wa matabaka yote Ijumaa ijayo wanatazamiwa kufanya maandamano ya nchi nzima kulaani ukatili unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika mji mtakatifu wa Quds na Msikiti wa al Aqsa sambamba na jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wa Rohingya.

Baraza la Uratibu na Uenezaji wa Kiislamu la Iran limesema jinai za jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina zimeingia katika hatua nyingine.

Baraza hilo limesema jinai hizo za Israel ni za kutisha, zisizofaa kunyamaziwa kimya na zinazostahili kulaaniwa na Waislamu na wapenda haki kote duniani.

Wapalestina wasipungua wanane wameuawa hadi sasa katika vurumai hizo katika Msikiti wa al-Aqsa.

Jinai dhidi ya Waislamu wa Rohingya

Kadhalika taarifa hiyo imeongeza kuwa, lengo jingine la maandamano hayo ya Wairani yatakayofanyika katika mikoa mitano ya Iran siku ya Ijumaa ni kukosoa jinai na madhila wanayoyapitia Waislamu wa Myanmar.

Kuanzia mwaka 2012 Waislamu wa Rohingya nchini Mynanmar zaidi ya elfu moja wameuawa na wengine zaidi ya laki moja kulazimishwa kuwa wakimbizi katika nchi jirani kutokana na ukandamizaji na mauaji ya umwagaji damu yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo ya kufurutu ada.