Dakta Larijani: Iran imejiandaa kukabiliana na vikwazo vipya vya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i32352-dakta_larijani_iran_imejiandaa_kukabiliana_na_vikwazo_vipya_vya_marekani
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, Iran imejiandaa kikamilifu kukabiliana na vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya taifa hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 27, 2017 23:03 UTC
  • Dakta Larijani: Iran imejiandaa kukabiliana na vikwazo vipya vya Marekani

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, Iran imejiandaa kikamilifu kukabiliana na vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya taifa hili.

Dakta Ali Larijani amebainisha kuwa, lengo la Marekani la kuiwekea vikwazo vipya Jamhuri ya Kiislamu ni kuleta hali ya mvurugiko baina ya wawekezaji wa kigeni na hivyo kuweka vizingiti vya uwekezaji nchini Iran.

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameashiria kupasishwa vikwazo vipya dhidi ya Iran na kueleza kuwa, lengo kuu la vikwazo hivyo ni kuanzisha vita vya kisaikolojia vyenye lengo la kukwamisha mwenendo wa uwekezaji hapa nchini.

Dakta Ali Larijani, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Dakta Larijani amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran sio jambo jipya na kwamba, athari yake itabakia katika makaratasi tu na kwamba, malengo ya vikwazo hivyo, zaidi ni ya kipropaganda. 

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameashiria nafasi muhimu na athirifu ya Iran katika matukio  ya eneo na katika vita dhidi ya ugaidi na kubainisha kwamba, kuiwekea vikwazo Iran ni jambo ambalo halina manufaa wala faida kwa Marekani na kwamba, taifa hili limejiandaa kikamilifu kukabiliana na vikwazo hivyo.

Aidha Larijani amesisitiza kwa mara nyingine tena kwamba, Iran haiwezi kusalimu amri mbele ya matakwa ya Marekani.