Zarif: Israel, tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i32562
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif ameutaja utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu na kutahadharisha kuwa, utawala huo bandia unafanya juu chini kuyayahudisha maeneo ya Palestina unayoyakaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 01, 2017 13:25 UTC
  • Zarif: Israel, tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif ameutaja utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni tishio kuu kwa ulimwengu wa Kiislamu na kutahadharisha kuwa, utawala huo bandia unafanya juu chini kuyayahudisha maeneo ya Palestina unayoyakaliwa kwa mabavu.

Zarif ameyasema hayo baada ya kuwasili mjini Istanbul nchini Uturuki, alikokwenda kushiriki mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) unaofanyika kufuatia kuongezeka ukandamizaji dhidi ya raia wa Palestina.

Dakta Zarif amesema: "Tishio kuu kwa umoja na mshikamano katika uliwengu wa Kiislamu ni utawala wa Kizayuni, ambao unachochea ugaidi na misimamo mikali katika eneo."

Kadhalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezitaka nchi za Kiislamu hususan katika eneo hili la Mashariki ya Kati kuwa macho kutokana na njama za maadui wao huku akieleza matumaini yake kuwa mkutano huo wa OIC utakuja na maazimio ambayo yataandaa uwanja wa kukomesha kikamilifu jinai za utawala pandikizi wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi.

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) 

Tangu tarehe 14 ya mwezi uliopita wa Julai, askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel walifunga milango ya msikiti wa Al-Aqsa na kuweka mageti ya elektroniki kwa ajili ya kuingilia msikiti humo, lakini hatimaye walilazimika kuyaondoa mageti hayo kutokana na malalamiko makubwa ya Wapalestina.

Wapalestina wasiopungua 10 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kushambuliwa na askari katili wa Israel katika msikiti huo, ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.