Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aelekea Muscat Oman
(last modified Mon, 02 Oct 2017 04:28:14 GMT )
Oct 02, 2017 04:28 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aelekea Muscat Oman

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran leo subuhi ameondoka Tehran na kuelekea ziarani mjini Muscat Oman kwa ajili ya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo na Qatar.

Akiwa mjini Muscat, Muhammad Javad Zarif atakuwa na mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Oman na Qatar na vile vile viongozi wa ngazi ya juu wa nchi mbili hizo. Masuala ya pande mbili, matukio ya kieneo na kimataifa yatajadiliwa katika ziara hiyo ya Zarif nchini Oman. 

Itakumbukwa kuwa, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliizuru Oman mwezi Februari mwaka huu ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikanda yenye lengo la kuboresha uhusiano na nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi na pia kujadili matukio mbalimbali katika eneo.

Rais Rouhani alipowasili M\uscat Oman mwezi Februari mwaka huu 

Ziara hiyo iliyofuatiwa na safari ya mwezi Julai ya Yusuf bin Alawi bin Abdullah Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman hapa Tehran ilijiri kufuatia kuibuka hali ya mivutano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na tawala za kiimla khususan Saudi Arabia.

 

 

 

Tags