Kikao cha Umoja wa Mabunge ya OIC kufanyika kesho Tehran
Kikao cha 38 cha Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) kitafanyika kesho Jumamosi kwenye makao makuu ya umoja huo hapa Tehran.
Tarehe ya kufanyika kikao cha maspika wa mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na vilevile ajenda ya mkutano huo ambao umepangwa kufanyika mwezi Januari mwakani hapa Tehran, itatangazwa katika kikao hicho cha 38 cha Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu (PUIC) kitakachofanyika kesho jijini Tehran.
Kikao hicho cha kesho kitachunguza masuala muhimu sana yanayohushu Ulimwengu wa Kiislamu ikiwemo kadhia ya Palestina, Syria na Iraq.
Nchi wanachama wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu (PUIC) kama Algeria, Azerbaijan, Benin, Cameroon, Indonesia, Lebanon, Msumbiji, Pakistan, Uturuki, Senegal, Mali na Iraq zitashiriki kikao hicho cha kesho hapa Tehran. Issaka Sidibe Spika wa Bunge la Mali ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo ya PUIC.
Dakta Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) atakutana na kuzungumza na washiriki wa kikao cha (PUIC) .