Iran katu haitafanya mazungumzo kuhusu uwezo wake wa makombora
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i35902-iran_katu_haitafanya_mazungumzo_kuhusu_uwezo_wake_wa_makombora
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitafanya mazungumo yoyote kuhusu makombora yake ya kujihami.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 24, 2017 01:01 UTC
  • Iran katu  haitafanya mazungumzo kuhusu uwezo wake wa makombora

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitafanya mazungumo yoyote kuhusu makombora yake ya kujihami.

Ayatullah Sadeq Amoli Larijani aliyasema hayo jana Jumatatu katika kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa vyombo vya mahakama. Huku akiashiria sera mpya zilizo dhidi ya Iran za serikali ya Marekani, Ayatullah Amoli Larijani amesema: "Iran imepata uzoefu mkubwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kama vile uungaji mkono (wa kigeni) kwa utawala wa Saddam katika vita vyake dhidi ya Iran na kwa msingi huo itatumia uwezo wake wote kujiimarisha ili iweze kujilinda na kujihami.

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema, nchi za Ulaya hazina haki ya kuingilia masuala ya kiulinzi ya Iran na kuoneza kuwa, mapatano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji JCPOA, hayawezi kutumiwa kuizuia Iran kujiimarisha katika sekta ya ulinzi.

Kombora la balistiki la Iran likifanyiwa majaribio

Ayatullah Sadeq Amoli Larijani pia amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapendwa na watu wa eneo na kwamba washauri wa kijeshi wa Iran wako Syria na Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali halali za nchi hizo za Kiarabu.

Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran ameashiria madai ya Marekani kuwa eti Iran inaunga mkono ugaidi na kusema: "Wamarekani waliingia Iraq kwa kisingizio cha kuleta amani nchini humo lakini baada ya kuharibu miundomsingi ya nchi hiyo walitekeleza mkakati wa kubakisha makundi ya kigaidi katika nchi hiyo lakini kwa himaya ya washauri wa kijeshi wa Iran na mrengo wa muqawama na mapambano,  njama hizo zimegonga mwamba.