Kashani: Umoja wa Walebanon umebatilisha njama za Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i36460-kashani_umoja_wa_walebanon_umebatilisha_njama_za_saudia
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa umoja na mshikamano wa taifa la Lebanon umebatilisha na kuzima njama za utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na Saudi Arabia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 17, 2017 13:17 UTC
  • Kashani: Umoja wa Walebanon umebatilisha njama za Saudia

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa umoja na mshikamano wa taifa la Lebanon umebatilisha na kuzima njama za utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani na Saudi Arabia.

Katika hotuba zake za Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, Ayatullah Muhammad Emami Mashani ameashiria tukio la kujiuzulu Waziri Mkuu wa Lebanon, Saad Hariri tena akiwa Riyadh nchini Saudi Arabia na kusema kuwa, suala hilo linaonesha kuwa, maadui wanapanga njama dhidi ya nchi za Waislamu na wanataka kuanzisha migogoro mingine katika eneo la Mashariki ya Kati hususan huko Lebanon.

Ameongeza kuwa, kwa baraka zake Mwenyezi Mungu, watu wa kaumu tofauti za Lebanon wamekwamisha na kubatilisha njama hizo.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amewashukuru Walebanon hususan Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah, Sayyid Hassan Hasrullah na kusema iwapo Hariri atarejea Lebanon atapokewa na Walebanon wote na suala hilo litakuwa na maana ya kubatilisha njama za watawala wa Saudi Arabia. 

Ayatullah Kashani

Ayatullah Kashani pia amezungumzia ukatili na jinai zinazoendelea kufanywa na utawala wa Aal Saudi katika eneo la Mashariki ya Kati hususan huko Yemen na kusema: Utawala wa Saudia ni dhalili na duni kiasi kwamba unaupatia fedha utawala haramu wa Israel ili uzishambulie nchi za Waislamu. 

Imamu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa, hali ya dunia ya sasa ni nyeti mno na amewataka Waislamu kuungana na kuwa macho mbele ya njama za maadui. 

Swala ya Ijumaa, Tehran

Vilevile amegusia tetemeko la ardhi lililoua mamia ya watu magharibi mwa Iran na kusema: Matamshi yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani akitaka isitolewe misaada ya kibinadamu kwa watu walioathiriwa na mtetemeko huo wa ardhi nchini Iran ni sauti chafu iliyotoka katika koo la mtu muovu. Ameongeza kuwa ni aibu na fedheha kwa dunia kuona Rais wa Marekani anatoa matamshi kama hayo.