Wapalestina wakaribisha uungaji mkono wa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i37525-wapalestina_wakaribisha_uungaji_mkono_wa_kamanda_wa_kikosi_cha_quds_cha_iran
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina amekaribisha kauli ya kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Meja Jenerali Qassem Suleimani ambaye ametangaza kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 13, 2017 00:20 UTC
  • Wapalestina wakaribisha uungaji mkono wa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Iran

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina amekaribisha kauli ya kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Meja Jenerali Qassem Suleimani ambaye ametangaza kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.

Jumatatu katika mazungumzo ya simu na kamanda wa Brigedi za Izzudin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Hamas na Kamanda wa Brigedi za Harakati ya Jihad Islami, Meja Jenerali Qassem Suleimani alitangza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kutoa uungaji mkono wa pande zote kwa harakati za Kiislamu za ukombozi wa Palestina.

Kufuatia kauli hiyo, Meja Jenerali Abu Ahmad Fuad, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina amesema: "Kwa kuzingatia kuwa Meja Jenerali Suleimani binafsi ni kamanda mwenye uzoefu katika medani ya vita, tunaunga mkono kauli yake."

Quds Tukufu

Fuad amesisitiza kuwa, leo harakati za muqawama na mapambano zina uwezo na nguvu zaidi ya huko nyuma na kuongeza kuwa: "Wapalestina hawako peke yao katika muqawama."

Aidha ametoa wito kwa makundi yote ya kupigania ukombozi wa Palestina yaungane ili yaweze kukabiliana na adui na jinai zake.

Halikadhalika ametoa wito kwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina inayoongozwa na Mahmoud Abbas ishiriki katika vikao vya Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina ili kukabiliana na uhasama uliotangazwa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Quds Tukufu.