Iran: Tutaendelea daima kutetea haki za taifa linalodhulumiwa la Palestina
Msaidizi maalumu wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) anayehusika na masuala ya kimataifa amesema katika mazungumzo yake na balozi wa Palestina hapa mjini Tehran kwamba Jahuri ya Kiislamu ya Iran daima itaendelea kupigania haki zilizoporwa za taifa la Palestina.
Hossein Abdullahiyan aidha amesema, siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote duniani hususan za Kiislamu.
Kwa upande wake, balozi wa Palestina mjini Tehran, Salah al Zawawi amegusia nafasi muhimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kupatikana amani na utulivu kwenye eneo hili la magharibi mwa Asia au Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa, mara zote Iran iko mstari we mbele katika juhudi za kuimarisha na kutia nguvu umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu.
Vile vile ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake wa kimaanawi kwa taifa la Palestina na kusema kuwa, ana imani thabiti kwamba taifa la wanamapambano la Palestina litapata ushindi katika mapambano yake.
Makundi na watu muhimu wa Palestina mara kwa mara huo huwa wanaishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake kwa wananchi wanaodhulumiwa kila upande wa Palestina.