Wananchi wa Iran waandamana na kulaani uadui wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i44342-wananchi_wa_iran_waandamana_na_kulaani_uadui_wa_marekani
Wananchi wa Iran wameandamana leo katika miji mbalimbali nchini baada ya Sala ya Ijumaa na kulaani vikali kuendelea uadui na ukiukaji ahadi wa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
(last modified 2026-04-29T03:42:39+00:00 )
May 11, 2018 09:58 UTC
  • Wananchi wa Iran waandamana na kulaani uadui wa Marekani

Wananchi wa Iran wameandamana leo katika miji mbalimbali nchini baada ya Sala ya Ijumaa na kulaani vikali kuendelea uadui na ukiukaji ahadi wa Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Wakiandamana baada ya ibada wa Sala ya Ijumaa wananchi hao kwa pamoja wamepaza sauti na kupiga nara ya "Mauti kwa Marekani" na kulaani uvunjaji ahadi wa Marekani pamoja na uadui wake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Maandamano hayo dhidi ya Marekani yamefanyika katika miji zaidi ya 950 ya Iran. Mjini Tehran pia maandamano hayo yalikuwa makubwa mno na waumini hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walipiga nara kuilaani serikali ya Marekani inayoongozwa na Rais Donald Trump.

Waandamanaji hao wametoa azimio mwishoni mwa maandamano yao wakitaka kutouamini pia Umoja wa Ulaya.

Maandamano dhidi ya Marekani baada ya Sala ya Ijumaa Tehran- 11/5/2018.

Sehemu moja ya azimio hilo inasema: Utafutaji visingizio na hatua za kiwendawazimu za Rais Donald Trump wa Marekani, kuzusha kwake vita vya kisaikolojia, kukiuka ahadi na kuchukua hatua ya upande mmoja ya kujiondoa katika makubaliano ya nyuklia sambamba na kutoa matamshi ya kipumbavu dhidi ya taifa lenye nguvu la Iran ni mambo ambayo yamethibitisha tena hali ya ubeberu na uistikabri waliyonayo  viongozi watenda jinai wa Marekani."

Aidha azimio hilo limeeleza katika sehemu nyingine kwamba, Marekani mtenda jinai hana lengo jingine bighairi ya kukabiliana na Uislamu, kufanya njama za kuupindua mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kuleta udhibiti wa kishetani katika eneo la Mashariki ya Kati.