Iran: Kamwe hatutorudi nyuma katika kuyaunga mkono mataifa yanayodhulumiwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i45102-iran_kamwe_hatutorudi_nyuma_katika_kuyaunga_mkono_mataifa_yanayodhulumiwa
Mkuu wa Chombo cha Mahakama cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Tehran kamwe haitolezegeza kamba katika kulinda malengo yake matukufu na thamani zake za kimsingi ikiwa ni pamoja na kuwaunga mkono wanyonge na kufanikisha malengo yake mengine ya Kiistratijia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 28, 2018 21:09 UTC
  • Iran: Kamwe hatutorudi nyuma katika kuyaunga mkono mataifa yanayodhulumiwa

Mkuu wa Chombo cha Mahakama cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Tehran kamwe haitolezegeza kamba katika kulinda malengo yake matukufu na thamani zake za kimsingi ikiwa ni pamoja na kuwaunga mkono wanyonge na kufanikisha malengo yake mengine ya Kiistratijia.

Ayatullah Sadeq Amoli Larijani alisema hayo jana (Jumatatu) katika kikao na maafisa wa ngazi za juu wa chombo hicho cha mahakama na huku akigusia namna Marekani ilivyojitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na wakati huo huo kuipangia Iran nini cha kufanya na nini cha kuacha amesema: Marekani inadhani kuwa imelitumbukiza taifa la Iran katika mgogoro mpya kumbe haijui kuwa, imefanya kosa kubwa kwani hatua kama hizo za Marekani ni jambo la kawaida kwa wananchi wa Iran.

Rais wa Marekani, Donald Trump

 

Amesema, ushetani wa viongozi wa Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ungali unaendelea na kufafanua kuwa: Uzoefu wa miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran bado haujawatosha viongozi wa Marekani na leo hii wamejitokeza kwa nguvu zao zote kujaribu kulivunja nguvu taifa la Iran.

Ameongeza kuwa, washauri wa serikali ya Marekani hivi sasa wana uhusiano wa karibu na magenge mabaya na khabithi zaidi ya kigaidi ulimwenguni na kwamba viongozi mafisadi kama hao wa Marekani hawawezi kamwe kulishinda taifa la Iran.

Licha ya Marekani kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA, lakini wafanikishaji wengine wa mapatano hayo ya kimataifa yaani Uingereza, Ufaransa, Russia, China, Ujerumani na Umoja wa Ulaya wote wanaendelea kuyaunga mkono.