Iran yaibuka mshindi katika mechi ya Kombe la Dunia na Morocco
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i45896-iran_yaibuka_mshindi_katika_mechi_ya_kombe_la_dunia_na_morocco
Timu ya Taifa ya Soka ya Iran imeibuka mshindi wa bao moja kwa nunge katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia na Morocco nchini Russia mjini St. Petersburg.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Jun 15, 2018 12:44 UTC
  • Iran yaibuka mshindi katika mechi ya Kombe la Dunia na Morocco

Timu ya Taifa ya Soka ya Iran imeibuka mshindi wa bao moja kwa nunge katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia na Morocco nchini Russia mjini St. Petersburg.

Bao la ushindi la Iran lilipachikwa wavuni kunako dakika ya 95 katika muda wa ziada ambapo mchezaji wa Morocco Azizi Bouhaddou alijifunga katika mechi hiyo ngumu. Ushindi huo ni wa kwanza wa Iran katika kombe la dunia tokea mwaka 1998. 

Morocco ilicheza vizuri katika dakika 30 za kwanza kabla ya Iran nayo ikaweza kuinuka na kupoteza nafasi ya kufunga kabla ya kumalizika nusu ya kwanza. Katika kipindi cha pili timu zote zilionekana kuwa na nguvu sawa na mechi ililikuwa inaelekea sare kabla la Morocco kujifunga.

Wachezaji wa Iran wakisherehekea ushindi

 Iran sasa inaongoza kundi B kwa pointi tatu . Timu zingine mbili katika kundi hilo ni Uhispania na Ureno ambazo zinacheza baadaye leo usiku katika mji wa Sochi.