Larijani: Iran iliingia katika mazungumzo ya nyuklia kulingana na misingi yake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i46414
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliingia kwenye mazungumzo na kundi la 5+1 kulingana na misingi na mbinu zinazofahamika; ambazo matokeo yake ilikuwa ni kufikiwa makubaliano ya nyuklia yaliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 28, 2018 08:02 UTC
  • Larijani: Iran iliingia katika mazungumzo ya nyuklia kulingana na misingi yake

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliingia kwenye mazungumzo na kundi la 5+1 kulingana na misingi na mbinu zinazofahamika; ambazo matokeo yake ilikuwa ni kufikiwa makubaliano ya nyuklia yaliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Akizungumza leo hapa Tehran, Ali Larijani ameashiria kuhusu malengo ya Iran ya kufanya mazungumzo hayo ya nyuklia na kuongeza kuwa kutoka katika kanuni ya saba ya Baraza la Usalama, kufungwa faili la PMD, na kuondolewa vikwazo vya nyuklia, yote hayo yalipelekea kufanyika mazungumzo kati ya Iran na kundi la 5+1 na kufikiwa makubaliano ya JCPOA, hata hivyo Marekani kwa upande mmoja imeamua kujitoa katika makubaliano hayo.  

Ali Larijani. Spika wa Bunge la Iran

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (bunge) amebainisha kuwa baada ya Marekani kujitoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, nchi hiyo imechukua hatua ya kuibua migogoro ya kisiasa, kiusalama na kuzusha mivutano nchini Iran kupitia mashinikizo ya kiuchumi ili kufanikisha malengo hayo. Ali Larijani amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa pigo kwa magaidi huko Syria na Iraq na kwamba iwapo hali isingekuwa hivi nchi zote za eneo hili zingekabiliwa na magaidi.