Iran na Russia kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i50695-iran_na_russia_kufanya_mazoezi_ya_pamoja_ya_kijeshi
Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran na Russia imepenga kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika Bahari ya Kaspi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 07, 2019 01:18 UTC
  • Iran na Russia kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi

Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran na Russia imepenga kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika Bahari ya Kaspi.

Admeri Hossein Khanzadi, Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mazoezi hayo yatajumuisha oparesheni za uokoaji na pia kukabiliana na uharami baharini. Aidha amesema Iran inapinga uwepo wa majeshi ya madola ajinabi katika eneo. Admeri Khanzadi amebaini kuwa, mazoezi hayo ya pamoja yatapalekea uhusiano wa kijeshi wa kistratijia wa Iran na Russia kuingia katika duru mpya. Halikadhalika amesema ushirikiano baina ya majeshi ya majini ya nchi za Bahari ya Kaspi unazidi kuimarika. Admeri Khanzadi amesisitiza kuwa majeshi ya kigeni hayaruhusiwi katika Bahari ya Kaspi na kuongeza kuwa bahari hii ni ya amani na urafiki na nchi zote za eneo zinazingatia sera hii.

Julai mwaka 2017 majeshi ya majini ya Iran na Russia yalifanya mazoezi ya pamoja katika Bahari ya Kaspi.

Meli ya kivita ya Iran ikifanya mazoezi

Hayo yamejiri wakati ambao Admeri Touraj Hassani-Moqaddam naibu kamanda wa jeshi la majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa kundi la manowari za jeshi hilo litaizunguka sayari ya dunia katika kipindi cha oparesheni zake mpya. Aliyasema hayo siku ya Ijumaa na kueleza kuwa manowari angamizi iitwayo "Sahand" inayobeba ndege itaandamana na manowari nyingine katika oparesheni hizo katika bahari ya Atlantiki.