Rais Rouhani: Ugaidi ni hatari kwa dunia nzima
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i508-rais_rouhani_ugaidi_ni_hatari_kwa_dunia_nzima
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa matukio ya miezi iliyopita yanaonyesha kuwa ugaidi ni hatari kwa wote ukiwemo Umoja wa Ulaya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2016 10:41 UTC
  •  Rais Rouhani: Ugaidi ni hatari kwa dunia nzima

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa matukio ya miezi iliyopita yanaonyesha kuwa ugaidi ni hatari kwa wote ukiwemo Umoja wa Ulaya.

Rais wa Iran ameyasema hayo leo hapa Tehran katika mazungumzo yake na Frank- Walter Steinmeier, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani aliyeko ziarani hapa nchini.

Amesisitiza kuwa suala la kuwapa magaidi vyanzo vya fedha na silaha linapasa kukomeshwa.

Rais wa Iran ameashiria pia nafasi chaya na muhimu ya Ujerumani katika mchakato wa mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 na kueleza kuwa, kutekelezwa kwa umakini na haraka makubaliano ya nyuklia (JCPOA) kuna maslahi kwa pande zote na katika uwanja huo juhudi zinapasa kufanyka ili kuimarisha zaidi misingi ya makubaliano hayo.

Rais Rouhani ameongeza kuwa, makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 nii kigezo mwafaka kilichotayarisha anga nzuri katika uwanja wa kimataifa kwa ajili ya kuweko maelewano na kujadili masuala mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesisitiza kuwa ukurasa mpya umefunguliwa katika uhusiano wa Umoja wa Ulaya na Iran kwa kutekelezwa rasmi makubaliano ya nyuklia (JCPOA) na kwamba Berlini imeazimia kuimarisha uhusiano wake na Tehran katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na katika vyuo vikuu. Steinmeier ameashiria pia safari zake mbili hapa Tehran katika muda wa miezi mitatu iliyopita na kusema kuwa ziara hizo zinaonyesha hamu ya Berilin ya kustawisha uhusiano wake na Tehran katika nyanja zote.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani aliyewasili jana mjini Tehran amezungumza pia na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif.