Rouhani: Waislamu wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i51612-rouhani_waislamu_wanapaswa_kuwa_na_umoja_na_mshikamano
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewahimzia Waislamu wote kuwa na umoja na mshikamano na kuwa na uhusiano wa kidugu na kirafiki kwa ajili ya kulinda usalama na amani yao.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Nov 29, -0001 20:34 UTC
  • Rouhani: Waislamu wanapaswa kuwa na umoja na mshikamano

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewahimzia Waislamu wote kuwa na umoja na mshikamano na kuwa na uhusiano wa kidugu na kirafiki kwa ajili ya kulinda usalama na amani yao.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo katika hadhara ya wananchi wa eneo la Bandar Lengeh huko kusini mwa Iran. Ameashiria shambulizi la kigaidi lililofanywa na kundi Jaishul Dhulm katika mkoa wa Sistan na Baluchestan huko kusini magharibi mwa Iran ambalo limeua shahidi askari 27 wa kulinda mpaka wa Iran na kusema kuwa: Taifa la Iran litalipiza kisasi cha damu ya mashahidi hao. 

Rais Rouhani amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaruhusu vibaka wanaopewa fedha na silaha na nchi za kigeni kuwaua shahidi walinzi wa mipaka yake. 

Amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa ikiimarisha amani na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na kamwe haijawahi kuanzisha vita dhidi ya nchi yoyote na kuongeza kuwa, Waislamu wanapaswa kuungana na kuimarisha umoja ili kulinda usalama na amani yao. 

Wakazi wa Bandar Lengeh wakimlaki Rais Rouhani

Amesema wale wanaodhani kuwa Marekani na Wazayuni wanalinda usalama wao wamo katika makosa makubwa na kusisitiza kuwa, kazi ya madola ya kibeberu ni kuzusha hitilafu na migawanyiko baina ya kaumu, madhehebu na mataifa mbalimbali na kwa msingi huo tunapaswa kuwa macho na makini. 

Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa, Iran ya Kiislamu itashinda na kubatilisha njama zote za maadui kwa kuimarisha umoja na kusimama kidete.