Khumalo: Afrika Kusini inafuatilia kupanuliwa mabadilishano ya kibiashara kati yake na Iran
(last modified Fri, 22 Feb 2019 08:03:45 GMT )
Feb 22, 2019 08:03 UTC
  • Khumalo: Afrika Kusini inafuatilia kupanuliwa mabadilishano ya kibiashara kati yake na Iran

Balozi wa Afrika Kusini hapa mjini Tehran amesema kuwa, kuna uwezo mkubwa mno katika sekta mbalimbali nchini Iran hususan katika uga wa madini, utalii na teknolojia ya mawasiliano na kwamba, nchi yake inaweza kuyatumia hayo kwa ajili ya kupanua zaidi ushirikiano kati yake na Iran.

Vika Mazwi Khumalo amesema hayo katika mazungumzo yake na Muhammad-Ali Talebi, Gavana wa Mkoa wa Yazd katikati mwa Iran na kueleza kwamba, uwepo wa uwezo wa kiutamaduni na kibiashara ni fursa ya dhahabu kwa ajili ya kupanuliwa zaidi ushirikiano baina ya nchi mbili hizi na kuwekezwa vitega uchumi katika mji wa Yazd.

Balozi wa Afrika Kusini nchini Iran amesema kuwa, licha ya kuwa, katika miaka ya hivi karibuni Marekani imeiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, lakini moja ya njia za kuvizunguka vikwazo hivyo ni kuweko mabadilishano ya kifedha na kustawishwa uhusiano wa kibiashara.

Vika Mazwi Khumalo, Balozi wa Afrika Kusini mjini Tehran akizungumza na Abbas Rezaei, Gavana Mkuu wa Isfahan, Abbas Rezaei,

Kwa upande wake, Muhammad-Ali Talebi, Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Yazd ameashiria katika mazungumzo yake  hayo na balozi Khumalo juu ya uwezo wa kiutamaduni, kiutalii, kiviwanda na kimadini wa mkoa huo kwa ajili ya kustawishwa zaidi ushirikkiano na Afrika Kusini na kusema kuwa, kuna nukta za pamoja kati ya Tehran na Pretoria ambazo zinapaswa kutumiwa kwa ajili ya kustawisha zaidi uhusiano kati ya pande mbili. 

Aidha akizungumza hapo jana na  Abbas Rezaei, Gavana Mkuu wa Isfahan, Abbas Rezaei, Balozi wa Afrika Kusini mjini Tehran alisema kuwa, hatua ya Marekani ya kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA haitapunguza ushirikiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyuga za uchumi, biashara na utamaduni.