Afrika yataka kupanua ushirikiano wa kielimu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i52100-afrika_yataka_kupanua_ushirikiano_wa_kielimu_na_jamhuri_ya_kiislamu_ya_iran
Kamishna wa Umoja wa Afrika Anayeshughulikia Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia amesema kuna haja ya kuweko ushirikiano wa kieliimu na Iran katika sekta ya teknolojia ya Nano, sayansi ya mazingira, teknolojia ya mawasiliano, kozi za stadi, ajira na uboreshaji wa kiwango cha elimu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 11, 2019 13:21 UTC
  • Afrika yataka kupanua ushirikiano wa kielimu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Kamishna wa Umoja wa Afrika Anayeshughulikia Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia amesema kuna haja ya kuweko ushirikiano wa kieliimu na Iran katika sekta ya teknolojia ya Nano, sayansi ya mazingira, teknolojia ya mawasiliano, kozi za stadi, ajira na uboreshaji wa kiwango cha elimu.

Bi Sarah Anyang Agbor, Kamishna wa Umoja wa Afrika Anayeshughulikia Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mazungumzo na Gholamreza Ansari, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Anayeshughulikia Masuala ya Uchumi na kuonyesha kuridhishwa na ustawi na maendeleo ya Iran katika nyanja mbalimbali za sayansi na teknolojia hususan uwepo mkubwa wa wanawake katika nyuga za elimu.

Sarah Agbor amesisitiza katika mazungumzo yake hayo na Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Anayeshughulikia Masuala ya Uchumi kwamba, Umoja wa Afrika una hamu na shauku kubwa ya kuwa na ushirikiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Iran na Afrika

Kwa upande wake Gholamreza Ansari, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Anayeshughulikia Masuala ya Uchumi ameashiria nafasi ya Iran katika uga wa elimu na teknolojia na kusema kuwa, ustawi na maendeleo yote haya ya kielimu ya Iran yamepatikana katika kipindi cha miaka 40 ya kuwekewa taifa hili vikwazo vya kidhulma.

Kadhalika Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran Anayeshughulikia Masuala ya Uchumi ameisifu misimamo ya Umoja wa Afrika kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).