Qassemi: Marekani imezuia misaada ya kibinadamu kuwafikia wahanga wa mafuriko nchini Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i52581
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Bahram Qassemi, amesema kuwa Marekani imefunga akaunti za Shirika la Hilali Nyekundu hatua ambayo ina maana ya kufunga mlango wa kutumwa misaada ya nchi tofauti za dunia kwa waathirika wa mafuriko yaliyoyakumba maeneo mbalimbali ya Iran.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 02, 2019 14:13 UTC
  • Qassemi: Marekani imezuia misaada ya kibinadamu kuwafikia wahanga wa mafuriko nchini Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Bahram Qassemi, amesema kuwa Marekani imefunga akaunti za Shirika la Hilali Nyekundu hatua ambayo ina maana ya kufunga mlango wa kutumwa misaada ya nchi tofauti za dunia kwa waathirika wa mafuriko yaliyoyakumba maeneo mbalimbali ya Iran.

Qassemi ameyasema hayo leo na kuongeza kwamba kitendo cha Marekani cha kufunga akaunti za Shirika la Hilali Nyekundu kimemfanya mtu yeyote aliye nje ya Iran kushindwa kufikisha msaada wake kwa ajili ya raia wa Iran waliokumbwa na mafuriko. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba hatua hiyo ya Washington ambayo imefanyika sawa na kukaribia tarehe ambayo Marekani ilijiondoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran JCPOA inawalenga raia wa kawaida wa Iran licha ya nara za kila mara na madai ya kipuuzi ya Marekani ambayo imekuwa ikisema kuwa vikwazo dhidi ya Iran haviwahusu wananchi.

Sehemu ya mafuriko yaliyoyakumba baadhi ya maeneo ya Iran

Aidha Qassemi amesema kuwa, kwa kawaida katika mazingira magumu na ya dharura, akaunti zote za benki huwa hazifungwi na badala yake huwa zinaachwa wazi kwa ajili ya kufikishwa misaada ya kibinaadamu kupitia asasi za kimataifa kama vile mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, lakini cha kushangaza ni kwamba, Marekani na katika hatua isiyo ya kibinaadamu na ya kidhalimu imefunga njia zote za ufikishaji misaada kwa wahanga wa mafuriko ya nchni Iran.

Amefafanua zaidi kwa kusema, jamii ya kimataifa na asasi za kimataifa zinatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kukomesha mienendo hiyo ya kinyama ya Marekani. Aidha amesisitiza kwamba Washington ni lazima ibebe dhima ya matokeo yote mabaya yatakayosababishwa na jinai yake ya kuzuia misaada ya kibinaadamu ya wahanga wa mafuriko nchini Iran.