Wanajeshi wa Israel wawauwa shahidi Wapalestina 77 katika siku moja pekee
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128626-wanajeshi_wa_israel_wawauwa_shahidi_wapalestina_77_katika_siku_moja_pekee
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa: Katika muda wa saa 24 zilizopita, raia 77 wa Palestina wameuawa shahidi na wengine 376 kujeruhiwa katika mashambulizi ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2025-07-22T10:14:58+00:00 )
Jul 22, 2025 10:14 UTC
  • Wanajeshi wa Israel wawauwa shahidi Wapalestina 77 katika siku moja pekee

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa: Katika muda wa saa 24 zilizopita, raia 77 wa Palestina wameuawa shahidi na wengine 376 kujeruhiwa katika mashambulizi ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza ongezeko la idadi ya wanaouliwa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kutangaza kuwa, raia 59,106 wa Palestina wameuawa shahidi tangu kuanza kwa mashambulizi na mauaji ya kimbari ya utawala wa kizayuni katika ukanda huo  7 Oktoba 2023. 

Wizara ya Afya ya Paletsina pia imetangaza kuwa Wapalestina 5 wameuwa shahidi na wengine 52 kujeruhiwa leo asubuhi wakati walipokuwa wakijaribu kufikia misaada ya kibinadamu. 

Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda a Gaza pia imeelezwa wasiwasi wake kuhusu hali ngumu ya ugawaji misaada ya kibiandamu na kutangaza kuwa idadi kadhaa ya wahanga bado wangali chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa kufutia mashambulizi ya Israel au miili ya wahanga hao imesalia katika mitaa mbalimbali; na wafanyakaiz wa huduma za uokoaji wanashindwa kuyafikia maeneo hayo kutokana na ukubwa wa mashambulizi.