Taarifa ya mwisho ya kikao cha kamisheni ya JCPOA yatolewa Vienna
Kamisheni ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA imetoa taarifa mwishoni mwa kikao chake huko Vienna na kutangaza kuwa wanachama wa JCPOA wanafanya jitihada za kufungua mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya, Instex mbele ya wadau wa masuala ya uchumi wa nchi nyingine.
Kamisheni ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA jana mwishoni mwa kikao hicho ilitangaza vipengee 9 ambapo nchi wanachama zimetilia mkazo umuhimu wa pande zote kuendelea kutekeleza kikamilifu na ipasavyo makubaliano hayo. Taarifa hiyo pia imekumbusha kuwa kuondolewa vikwazo ni sehemu muhimu ya makubaliano hayo ya kimataifa. Nchi hizo aidha zimetazama upya majukumu na ahadi zao kuhusiana na makubaliano ya JCPOA. Taarifa ya mwisho ya kikao cha kamisheni ya JCPOA imesisitiza pia nafasi muhimu ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) kama taasisi pekee isiyoegemea upande wowote na inayosimamia utekelezaji wa masuala yanayohusiana na miradi ya nyuklia ya Iran kama ilivyoainishwa katika makubaliano ya JCPOA na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kikao cha kamisheni ya makubaliano ya JCPOA chini ya Mwenyekiti wake Sayyid Abbas Arachi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Helga Schmid Naibu Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya, Manaibu na Wakurugenzi Wakuu wa Kisiasa wa Iran na wa kundi la 4+1 linaloundwa na Ujerumani, Ufaransa, Russia, China na Uingereza kilimaliza shughuli zake jana huko Vienna, Austria.
Kutekelezwa mfumo wa INSTEX ilikuwa miongoni mwa habari umuhimu sana zilizotangazwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani hiyo jana baada ya kumalizika.
baada ya kumalizika kikao hicho Helga Schmid, Msaidizi wa Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, alisema kuwa mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya, tayari umeanza kufanya kazi na hatua ya kwanza ya mabadilishano hayo inaendelea kufanya kazi.