Dakta Kharrazi: Kukombolewa Palestina ni miongoni mwa malengo makubwa ya Iran
Mkuu wa Baraza la Kiistratijia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kukombolewa Palestina na mji mtakatifu wa Quds ni katika malengo makkuubwa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Dakta Kamal Kharrazi amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika mazungumzo yake na Saleh al-Arouri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kusisitiza juu ya azma ya Iran ya kuendelea kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina.
Kwa upande wake, Saleh al-Arouri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa himaya, uungaji mkono wake na misimamo yake thabiti kuhusiana na kadhia nzima ya Palesta.
Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, ana matumaini kwamba, uhusiano na ushirikiano wa kidugu wa Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran na Palestina utaendelea mpaka mji mtakatifu wa Quds utakapokombolewa kutoka mikononi mwa maghasibu Wazayuni.
Ujumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ukiongozwa na Saleh al-Arouri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati hiyo uliwasili jana hapa mjini Tehran kwa shabaha ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.