Msimamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu jinai za utawala wa Bahrain
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55107-msimamo_wa_kiongozi_muadhamu_kuhusu_jinai_za_utawala_wa_bahrain
Ofisi ya Kulinda na Kusambaza Athari za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza msimamo wa Ayatullah Ali Khamenei kuhusu jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Khalifa huko Bahrain baada ya utawala huo kuwaua shahidi vijana wawili wa nchi hiyo kwa tuhuma bandia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 31, 2019 11:11 UTC
  • Msimamo wa Kiongozi Muadhamu kuhusu jinai za utawala wa Bahrain

Ofisi ya Kulinda na Kusambaza Athari za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza msimamo wa Ayatullah Ali Khamenei kuhusu jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Khalifa huko Bahrain baada ya utawala huo kuwaua shahidi vijana wawili wa nchi hiyo kwa tuhuma bandia.

Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu jinai ya hivi karibuni ya utawala wa Bahrain umesema: "Dhulma na ukandamiaji haviwezi kudumu na hatimaye azma na irada madhubuti ya mataifa yanayopigania uadilifu itashinda na kuibuka kidedea."

Ayatullah Ali Khamenei amekuwa akikemea na kulaani jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na utawala wa kiimla wa ukoo wa Aal Khalifa nchini Bahrain ukisaidiwa na Saudi Arabia dhidi ya wananchi wanaotaka mageuzi na utawala utakaochaguliwa na wananchi wenyewe. 

Ali al-Arab na Ahmad al-Malali walinyongwa kwa tuhuma zisizo na msingi.

Vijana Ali al-Arab, 25, na Ahmad al-Malali, 24, wa Bahrain walinyongwa siku kadhaa zilizopita kwa tuhuma bandia za eti kumuua afisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo. 

Utawala wa kiimla wa Aal-Khalifa umewanyonga vijana hao licha ya mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiwemo ya Amnesty International na Human Rights Watch pamoja na Umoja wa Mataifa kutoa miito ya kutaka kusimamishwa utekelezaji wa adhabu hiyo ya kifo.