Mwakilishi wa Hamas Iran asisitiza kuhusu umoja wa nchi za Kiislamu
(last modified Thu, 10 Oct 2019 04:25:45 GMT )
Oct 10, 2019 04:25 UTC
  • Mwakilishi wa Hamas Iran asisitiza kuhusu umoja wa nchi za Kiislamu

Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nchini Iran ametoa wito wa Umoja wa nchi za Kiislamu katika kukabiliana na maadui.

Khaled al-Qaddumi, mwakilishi wa Hamas nchini Iran aliyasema hayo Jumatano mjini Bushehr kusini mwa Iran alipohutubu katika 'Kikao cha Tano cha Kitaalamu Kuhusu Haki za Binadamu za Kimarekani kwa Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu'. Al Qaddumi ameongeza kuwa 'Marekani na utawala ghasibu wa Israel ambao unakalia Quds Tukufu kwa mabavu, haziwatakii mema watu wa eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati)'.

Afisa huyo wa Hamas amebaini kuwa, uzoefu wa mwamko wa watu wa eneo la Asia Magharibi umeonysha kuwa, ubeberu na uistikbari wa kimataifa ungali unaunga mkono madikteta na tawala za kiimla ili matakwa ya wananchi yasiweze kufikiwa.

Kikao cha Tano cha Kitaalamu Kuhusu Haki za Binadamu za Kimarekani kwa Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mwakilishi wa Hamas nchini Iran amebaini kuwa, leo hatari ya utawala wa Kizayuni wa Israel inahisika katika miji mikuu yote ya nchi za eneo. Ameongeza kuwa: "Kusimama kidete mbele ya utawala wa Kizayuni ni kulinda usalama wa umma wa Kiislamu".

'Kikao cha Tano cha Kitaalamu Kuhusu Haki za Binadamu za Kimarekani kwa Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu' kilifanyika jana Jumatano katika mji wa Bushehr kusini mwa Iran.

 

 

Tags