Muosavi: Iran inafuatilia kwa makini matukio ya Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56883-muosavi_iran_inafuatilia_kwa_makini_matukio_ya_iraq
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kusikitishwa kwake na yanayojiri katika nchi jirani ya Iraq ambayo yamepelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya watu na kuharibiwa mali ya umma na kusema: Tehran inafuatilia kwa makini yanayojiri nchini humo.
(last modified 2026-02-22T02:21:18+00:00 )
Oct 27, 2019 07:32 UTC
  • Muosavi: Iran inafuatilia kwa makini matukio ya Iraq

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza kusikitishwa kwake na yanayojiri katika nchi jirani ya Iraq ambayo yamepelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya watu na kuharibiwa mali ya umma na kusema: Tehran inafuatilia kwa makini yanayojiri nchini humo.

Sayyid Abbas Mousavi amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono matakwa ya wananchi wa Iraq yaliyoelezwa kupitia taarifa na matamshi za viongozi wa kidini na Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul-Mahdi. 

Mousavi ameeleza masikitiko yake makubwa kutokana na matukio ya sasa huko Iraq na ghasia zinaoendelea kushuhudiwa nchini humo na kusema: Tehran ina matumaini kwamba serikali, taifa la Iraq na viongozi wakuu wa kidini wanaweza kupata suluhisho la machafuko hayo na kuijenga nchi kwa ushirikiano. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, tangu baada ya kuanzishwa Iraq mpya, Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa pamoja na serikali na taifa la nchi hiyo katika vipindi vyote nyeti na imetoa suhula na misaada yake yote kwa nchi rafiki, ndugu na jirani ya Iraq. 

Iraq

Katika wiki za hivi karibuni baadhi ya mikoa ya Iraq imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali mbaya ya huduma za kijamii, ukosefu wa ajira na ufisadi katika idara za serikali. Maandamano hayo yameambatana na machafuko yaliyosababisha mauaji na kujeruhiwa makumi ya watu.