Iran na China zafanya mazungumzo kuhusu JCPOA
(last modified Sun, 01 Dec 2019 07:21:19 GMT )
Dec 01, 2019 07:21 UTC
  • Iran na China zafanya mazungumzo kuhusu JCPOA

Iran na China zimekutana katika kikao cha mashauriano kuhusu namna ya kulinda vipengee vya mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Kikao hicho kimefanyika mapema leo Jumapili baina ya Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika masuala ya siasa na Ma Jao Shi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China.

Sayyid Araqchi amesema kuwa, Tehran na Beijing ni washirika wa kiistratijia na ndio maana leo pande hizo mbili zimekutana kwenye kikao maalumu cha kujadili masuala muhimu ya kieneo na kimataifa. Amesema amefurahi kuona mazingira mazuri yameandaliwa hivi sasa ya kuweza kufanyika kikao kama hicho.

Sayyid Abbas Araqchi (kushoto) akiwa na Ma Jao Shi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China

 

Kwa upande wake, Ma Jao Shi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China amesema kuwa, Iran ni mshirika wa kiistratijia wa nchi yake. Amesema, China ina hamu ya kuimarisha zaidi na zaidi uhusiano wake na Iran katika masuala yote ya kieneo na kimataifa yakiwemo mambo yanayozihusu nchi mbili kama vile mapatano ya nyuklia ya JCPOA. Amesema lengo kuu la uhusiano huo mzuri baina ya Iran na China ni kuimarisha usalama na amani kieneo na kimataifa.

Manaibu Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na China wamebadilishana mawazo pia kuhusu kikao cha kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya JCPOA kitakachowakutanisha pamoja Manaibu Mawaziri wa pande zilizobakia ndani ya mapatano hayo ya kimataifa. Kikao hicho kitafanyika mjini Vienna, Austria. 

Tags