Sayyid Abbas Araqchi: Mashauriano baina ya Iran na Japan yataendelea
(last modified Sat, 21 Dec 2019 13:37:57 GMT )
Dec 21, 2019 13:37 UTC
  • Sayyid Abbas Araqchi: Mashauriano baina ya Iran na Japan yataendelea

Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema kuwa, mashauriano ya kisiasa kati ya Iran na Japan yataendelea.

Akibainisha kuhusiana na safari ya Rais Hassan Rouhani nchini Japan pamoja na mazungumzo yake na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo, Sayyid Abbas Araqchi ameeleza kwamba, mazungumzo kati ya pande mbili yalijikita zaidi katika masuala ya pande mbili, kieneo na kimataifa. 

Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema kuwa, viongozi wa Iran na Japan walijadiliana kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA pamoja na vikwazo vya Marekani.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran asubuhi ya jana Ijumaa aliwasili Tokyo mji mkuu wa Japan akiitikia mwaliko wa Abe Shinzo, Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Mazungumzo ya Rais Hassan Rouhani na Abe Shinzo, Waziri Mkuu wa Japan

Katika mazungumzo yake na Abe Shinzo, Rais Rouhani alibainisha kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kueleza kwamba, Iran imefanya kila jitihada ili kuyalinda makubaliano hayo katika fremu ya kudhamini maslahi yake na itaendelea kufanya hivyo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Japan alieleza kufurahishwa na safari ya Rais wa Iran ya kuitembelea nchi hiyo na kusisitiza kuwa nchi yake ina hamu kubwa ya kupanua uhusiano na Tehran katika nyanja zote.  Hadi tunaingia mitamboni, Raiis Rouhani alikuwa ameondoka Tokyo na kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Tags