Rais Rouhani: Marekani haina ubavu wa kulipigisha magoti taifa imara la Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62414-rais_rouhani_marekani_haina_ubavu_wa_kulipigisha_magoti_taifa_imara_la_iran
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani pamoja na majigambo yake haina ubavu wa kulipigisha magoti taifa la Iran na kulifanya lifuate matakwa yake.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jul 25, 2020 06:58 UTC
  • Rais Rouhani: Marekani haina ubavu wa kulipigisha magoti taifa imara la Iran

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani pamoja na majigambo yake haina ubavu wa kulipigisha magoti taifa la Iran na kulifanya lifuate matakwa yake.

Rais Rouhani amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika kikao cha kikao cha Kamati ya Taifa ya Kupamabana na virusi vya Corona hapa nchini ambapo ameashiria njama za maadui zenye lengo la kutoa pigo kwa taifa hili na kusema kuwa, wananchi wa Iran wana nguvu na uwezo wa kutosha wa kukabiliana na njama za maadui.

Rais Rouhani amesema kwamba, wananchi wa Iran wako imara na wanaweza kukabiliana kikamilifu na mashinikizo ya maadui na katu hawatapiga magoti na kusalimu amri mbele ya maadui wa taifa hili.

Kadhalika Rais Hassan Rouhani amebainisha kuwa, wananchi wa Iran wanatoa ushirikiano kikamilifu na katu hawazembei katika kukabiliana na vikwazo, virusi vya Corona au tatizo jingine lolote lile kubwa.

Dakta Rouhani sambamba na kubainisha anga ya kustafidi na mipango ya kitaifa iliyopo hapa nchini licha ya vikwazo vya maadui kinara wao akiwa Marekani ameeleza kwamba, hii inaonyesha kuweko harakati ya taifa katika njia ya ustawi na maendeleo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamju ya Iran amesema bayana kwamba, ana matumaini na mustakabali mzuri ambapo kuweko mipango mizuri na imara, ni njia bora ya kuyapatia ufumbuzi na kufikia mustakabali mwema na mzuri.