Iran: Uwepo wa US katika Ghuba ya Uajemi unasababisha ukosefu wa usalama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i6403-iran_uwepo_wa_us_katika_ghuba_ya_uajemi_unasababisha_ukosefu_wa_usalama
Ofisa mwandamizi wa jeshi la majini la Iran amesema uwepo wa majeshi ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman unapania kusababisha ukosefu wa usalama na kueneza harakati za kigaidi katika eneo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 04, 2016 10:03 UTC
  • Iran: Uwepo wa US katika Ghuba ya Uajemi unasababisha ukosefu wa usalama

Ofisa mwandamizi wa jeshi la majini la Iran amesema uwepo wa majeshi ya Marekani katika Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman unapania kusababisha ukosefu wa usalama na kueneza harakati za kigaidi katika eneo.

Admeli Reza Abbasi amesema: "Vikosi hivyo vya Marekani havina sababu ya msingi ya kuwepo katika Ghuba ya Uajemi ghairi ya kusababisha ukosefu wa usalama, kueneza ugaidi, ujasusi na kueneza propaganda na chuki dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Admeli Abbasi ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kujiimarisha kijeshi na kusisitiza kuwa, uwepo wa majeshi ya Iran katika Ghuba ya Uajemi ni kwa lengo la kukabiliana na chokochoko za maadui sambamba na kulinda maji ya nchi hii. Amesisitiza kuwa, Iran itaendelea kufanya luteka na kuimarisha uwezo wake wa kijeshi ili kuhakikisha kuwa jeshi la majini la Iran linakuwa tayari kujibu uchokozi wowote wa adui.

Matamshi ya afisa huyo mwandamizi wa jeshi la baharini la Iran yamekuja siku chache baada ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kukosoa uwepo wa vikosi vya Marekani katika Ghuba ya Uajemi. Jumatatu iliyopita, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema: "Ghuba ya Uajemi ni nyumbani kwa taifa la Iran na pwani za ghuba hiyo na maeneo ya Bahari ya Oman ni milki ya taifa hili adhimu, lazima tuwe macho katika maeneo hayo, tufanye mazoezi ya kijeshi ili kudhihirisha uwezo wetu, hivyo Marekani ndiyo inayopasa kufafanua ni kwa nini imekuja kutoka upande ule wa dunia kufanya luteka zao hapa."