Ayatullah Akhtari: Kubakia nyuma kiuchumi ni natija ya kuanzisha uhusiano na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64440-ayatullah_akhtari_kubakia_nyuma_kiuchumi_ni_natija_ya_kuanzisha_uhusiano_na_israel
Mkuu wa Kamati ya Kuunga Mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Wananchi wa Palestina katika Ofsi ya Rais wa Iran amesema kuwa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel hakuna jingine isipokuwa kukandamizwa na kubakia nyuma kiuchumi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 05, 2020 04:47 UTC
  • Ayatullah Akhtari: Kubakia nyuma kiuchumi ni natija ya kuanzisha uhusiano na Israel

Mkuu wa Kamati ya Kuunga Mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Wananchi wa Palestina katika Ofsi ya Rais wa Iran amesema kuwa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel hakuna jingine isipokuwa kukandamizwa na kubakia nyuma kiuchumi.

Ayatullah Muhammad Hassan Akhtari leo amesema kuwa, Wasudani wanapinga kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na wanasisitiza kufungamana na thamani za Kiislamu. Ayatullah Akhtari amesema kuwa, mchakato wa kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni una lengo la kuyakandamiza mataifa mengine kwa kuziondoa madarakani serikali halali na kuziingiza  batili.    

Mkuu wa Kamati ya Kuunga Mkono Mapinduzi ya Kiislamu ya Wananchi wa Palestina katika Ofisi ya Rais wa Iran ameongeza kuwa: ni wazi kuwa matokeo ya hatua hiyo si kingine ghairi ya udhalilishaji na kubaki nyuma kiuchumi kutokana na uchambuzi na tathmini ya kimaidani kuhusu nchi ambazo zimekuwa na uhusiano na utawala wa Kizayuni.  

Utawala wa Kizayuni na serikali ya mpito ya Sudan hivi karibuni zilitoa taarifa ya pamoja kuhusu kuanzisha uhusiano kati ya pande mbili hizo. Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na Bahraina pia Septemba 15 mwaka huu zilisaini mapatano ya kuanzisha uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni huko White House katika hafla iliyohudhuriwa na Rais Donald Trump wa Marekani na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu.   

Serikali za Kiarabu zinafanya jitihada za kuanzisha uhusiano rasmi na Israel katika hali ambayo utawala huo ghasibu mbali na kuwakandamiza wananchi wa Palestina umeyakalia kwa mabavu maeneo mengi ya Waarabu na  Waislamu. 

Ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni