Rais Rouhani: Kwa mara nyingine tena, Iran imeipiga mweleka Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i66466-rais_rouhani_kwa_mara_nyingine_tena_iran_imeipiga_mweleka_marekani
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ya kukataa pingamizi la Marekani kuhusu mashataka ya Tehran dhidi yake, ni ushindi mwingine kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2021 09:25 UTC
  • Rais Rouhani: Kwa mara nyingine tena, Iran imeipiga mweleka Marekani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ya kukataa pingamizi la Marekani kuhusu mashataka ya Tehran dhidi yake, ni ushindi mwingine kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo na kuongeza kuwa, licha ya Marekani kutumia maelfu ya wataalamu wa fani mbalimbali kuendesha vita vya kisiasa dhidi ya Iran, na licha ya taifa hili la Kiislamu kuingia katika vita hivyo likiwa na idadi ndogo tu ya wanadiplomasia wake lakini limeishinda Marekani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha amesema, kabla ya hapo na katika mashataka yaliyofunguliwa na Tehran katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC dhidi ya Marekani kutokana na vikwazo vyake vya kidhulma, na licha ya Marekani kutumia maelfu ya wanasheria kujaribu kukwamisha mashtaka hayo lakini imeshindwa.

Mshikamano wa wananchi wa Iran

 

Mahakama hiyo imetoa hukumu ya kuiwajibisha Marekani kufuta mara moja vikwazo vyake vyote vinavyohusiana na masuala ya kibinadamu. Tab'an isipotekeleza amri hiyo ya mahakama, Marekani itakuwa imeongeza jinai yake nyingine katika faili la jinai zake zisizo na idadi katika pembe mbalimbali za dunia.

Amesema, katika hatua hii Marekani imefanya njama ya kuthibitisha kuwa mahakama ya ICC haiwezi kisheria kusikiliza kesi hiyo ya Iran. Hata hiyo jana Jumatano mahakama hiyo ilitoa hukumu ya kupinga pingamizi hilo la Marekani na hayo ni mafanikio makubwa ya kisheria kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ushindi huo unaonesha kuwa taifa kubwa la Iran na vijana wake wasomi wako imara katika nyuga za kidiplomasia, za kisheria na masuala ya kiufundi.