Zarif akosoa siasa za kindumakuwli na kibaguzi za Ufaransa
(last modified Thu, 29 Apr 2021 09:54:04 GMT )
Apr 29, 2021 09:54 UTC
  • Javad Zarif
    Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhurii ya Kiislamu ya Iran amezungumzia majaribio ya makombora yaliyofanywa na Ufaransa na juhudi za Paris na baadhi ya nchi za Magharibi za kutaka kubana miradi ya kutengeneza makombora ya Iran na kuandika kuwa; Inaonekana kuwa, siasa za kibaguzi na kindumakuwili ni jambo linalowezekana.

Akiashiria majaribio hayo ya makombora yaliyofanywa na Ufaransa, Muhammad Javad Zarif ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: "Kidhahiri sera za kibaguzi na kindumakuwili zinawezekana." Maandishi hayo ya Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran yameambatanishwa na mkanda wa video wa majaribio ya kombora la kistratijia la M51.2 yaliyofanywa na Ufaransa. 

Jeshi la Ufaransa mapema Jumatano ya jana lilifanyia majaribio kombora la kistratijia la balestiki la M51.2 katika kituo cha  Biscarosse pwani mwa bahari ya Atlantic. Kombora hilo linasanifiwa katika uwezo wa silaha za nyuklia.

Majaribio la kombola la M51.2

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Vikosi vya Jeshi la Ufaransa imedai kuwa, majaribio hayo yamefanyika kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa.    

Itakumbukwa kuwa Ufaransa ni miongoni mwa nchi za Magharibi zinazodai kuwa, miradi ya kutengeneza makombora ya Iran inapaswa kujadiliwa kwenye meza ya mazungumzo na kuwekewa mipaka.