Iran ina nafasi muhimu katika kudumisha usalama wa Ghuba ya Uajemi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i69610-iran_ina_nafasi_muhimu_katika_kudumisha_usalama_wa_ghuba_ya_uajemi
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi muhimu katika kudumisha usalama katika eneo zima la Ghuba ya Uajemi. Hayo yamesemwa na Shahriar Heidari Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Usalama wa Taifa katika Bunge la Iran.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Apr 30, 2021 06:46 UTC
  • Iran ina nafasi muhimu katika kudumisha usalama wa Ghuba ya Uajemi

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi muhimu katika kudumisha usalama katika eneo zima la Ghuba ya Uajemi. Hayo yamesemwa na Shahriar Heidari Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Usalama wa Taifa katika Bunge la Iran.

Katika mahojiano na Iran Press, Heidari amesema  mbali na kuwa hivi sasa asilimia kubwa ya nishati ya dunia inatoka eneo la Ghuba ya Uajemi, eneo hili kwa muda mrefu limekuwa na mvuto duniani kutokana na nafasi yake muhimu kwa mtazamo wa jiografia ya kisiasa.

Aidha amesisitiza kuhusu umuhimu wa Lango Bahari la Hormuz katika Ghuba ya Uajemi na kusema lango hilo ni njia muhimu ya meli na lina nafasi nyeti katika kufikisha nishati maeneo yote ya dunia. Aidha amesema Lango Bahari la Hormuz ni kati ya malango saba muhimu ya bahari duniani.

Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Usalama wa Taifa katika Bunge la Iran amesema kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina nafasi muhimu katika usimamizi wa Lango Bahari la Hormuz. Hali kadhalika amesema madola makubwa duaniani yanaibua taharuki katika eneo la Ghuba ya Uajemi kwa lengo la kupora utajiri wa mafuta na gesi katika eneo hilo.

Meli ya kivita ya Iran ikifanya mazoezi katika Ghuba ya Uajemi

Amesema Iran haitaruhusu madola ya kigeni yavuruge usalama wa Ghuba ya Uajemi na kwamba  majeshi ya majini ya Iran yanaimarisha uwezo wao kwa ajili ya kudumisha usalama katika eneo hilo.

Ikumbukwe kuwa, leo tarehe 10 Ordebehesht kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani sawa na tarehe 30 Aprili, inafahamika kuwa siku ya kitaifa ya Ghuba ya Uajemi. Siku hii iliitwa siku ya kitaifa ya Ghuba ya Uajemi kutokana na baadhi ya pande zenye chuki dhidi ya Iran, kufanya njama za kutaka kupotosha historia, kwa kuiita kwa majina mengine yasiyo na msingi. Jina la kihistoria la Ghuba ya Uajemi limetafsiriwa katika lugha mbalimbali kwa jina hilo au kwa jina la Bahari ya Pars.