Mdahalo wa Pili wa Urais nchini Iran unafanyika leo
Mdahalo wa pili wa wagombea wa urais nchini Iran unafanyika alasiri ya leo mwendo wa saa kumi na moja kwa saa za hapa nchini, kupitia televisheni na radio za taifa.
Mdahalo wa leo unatazamiwa kujikita zaidi katika masuala ya utamaduni, kijamii na kisiasa, kuelekea uchaguzi wa rais utakaofanyika katika kipindi cha siku 10 sijazo.
Mdahalo wa kwanza ulifanyika Jumamosi iliyopita ya Juni 5, huku wa tatu na wa mwisho ukiratibiwa kufanyika Jumamosi ijayo ya tarehe 12 Juni.
Wagombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu nchini Iran ni Saeed Jalili, Mohsen Rezaee Mirgha'ed, Sayyid Ebrahim Raisi, Alireza Zakani, Sayyid Amir-Hossein Ghazizadeh Hashemi, Mohsen Mehralizadeh na Abdolnaser Hemmati.
Rais wa sasa Hassan Rouhani anakamilisha muhula wake wa pili mfululizo na hivyo haruhusiwi kugombea awamu hii kisheria.
Uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uchaguzi wa 6 wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya tarehe 18 mwezi huu wa Juni, 2021.