Rais Rouhani asisitiza kuimarishwa uhusiano wa Iran na Kenya
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitia kuimarisha uhusinao baina ya nchi mbili za Iran na Kenya wakati alipopokea hati ya utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Kenya mjini Tehran.
Rais anayemaliza muda wake wa Iran amepongeza uhusiano wa Iran na Kenya na kuitaja Kenya kuwa lango kuu la kuingizia bidhaa za Iran kuelekea katika masoko ya nchi mbalimbali barani Afrika.
Katika mazungumzo hayo ya leo na balozi mpya wa Kenya mjini Tehran, Rais Hassan Rouhani amesema kuwa Iran na Kenya zimekuwa na uhusiano mwema na wa amani na kusisitiza juu ya haja ya kuimaishwa uhusiano wa nchi mbili katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kisayansi.
Baada ya kupokea hati ya utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Kenya, Rais Rouhani amesema kuwa, kuna mazingira mazuri na suhula kwa ajili ya kuimarisha uhusiano kati ya Tehran na Nairobi. Kwa upande wake Joshua Igweta Gatimu balozi mpya wa Kenya mjini Tehran ameashiria uhusiano mkongwe na unaokua baina ya Kenya na Iran na kusema, lengo lake kuu akiwa balozi hapa ni kupanua zaidi uhusiano wa pande mbili.